Katika hotuba yake, Dkt. Kamal Sheriff alitumia methali mashuhuri, “Tembo wawili wanapopigana, ni nyasi zinazoumia,” kufafanua changamoto zinazojitokeza katika familia, jamii, na hata katika uongozi wa kitaifa na kimataifa. Ufafanuzi wake uliweka wazi namna migogoro ya juu inavyoathiri watu wa kawaida na umuhimu wa kujenga nafasi endelevu za amani na uwajibikaji.

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt as -ABNA- Dar-es-salaam, Falah Islamic Development (FID) imefanya Kikao muhimu siku ya Alkhamisi ambacho kimefanyika kwa mafanikio makubwa na kilijaa mafunzo yenye umuhimu mkubwa kwa jamii. Kikao hicho kilihusu masuala ya Kijamii na umuhimu wa kuilinda na kuitunza Amani ya Nchi. Vijana wengi wa Kizazi Kipya walipata fursa ya kuhudhuria katika Kikao hiki na kusikiliza Hotuba Muhimu iliyogusia Changamoto za Kijamii na kifamilia na Nafasi ya Amani katika Maendeleo ya Kijamii na kifamilia na Taifa kwa ujumla.
Katika hotuba yake, Dkt. Kamal Sheriff alitumia methali mashuhuri, “Tembo wawili wanapopigana, ni nyasi zinazoumia,” kufafanua changamoto zinazojitokeza katika familia, jamii, na hata katika uongozi wa kitaifa na kimataifa. Ufafanuzi wake uliweka wazi namna migogoro ya juu inavyoathiri watu wa kawaida na umuhimu wa kujenga nafasi endelevu za amani na uwajibikaji.
Waumini na washiriki waliokuwepo walitoa mchango mkubwa katika kujadili na kufafanua masuala mbalimbali, na kufanya kikao hiki kuwa chenye matokeo chanya.

Falah Islamic Development imeelezea shukrani kwa wote waliohudhuria na kushiriki kikamilifu, na imesisitiza kuwa malengo ya vikao hivi ni kuandaa jamii kuwa chachu ya amani, uponyaji, na uongozi bora.
FID imethibitisha kuwa vikao vingine vyenye athari na manufaa zaidi vitaendelea kufanyika, InshaAllah.

Your Comment